- 131 viewsDuration: 3:08Kenya imetangaza kwamba imekuwa taifa la kwanza barani Afrika kujiunga na mpango wa afya wa kimataifa. Mpango huo wa miaka mitano unaolenga kupunguza vifo vya watoto wachanga utagharimu takriban shilingi bilioni 11 na utatekelezwa katika kaunti 12 ambazo zinachangia asilimia 50 ya vifo vya watoto wachanga nchini. Na kama anavyoarifu Emily Chebet, kaunti ya Nakuru itakuwa ya kwanza kutekeleza mradi huo.