- 3,436 viewsDuration: 3:39Baadhi ya wanasiasa wa Kenya Kwanza, wakiongozwa na naibu rais Kithure Kindiki, wamesuta upinzani unaoongozwa na kinara wa DCP Rigathi Gachagua pamoja na mrengo wa Linda Wananchi, na kuwataka kuacha kumhusisha rais William Ruto na kupanda kwa bei ya mafuta. Serikali imesema inafanya kila iwezalo kudhibiti bei ya bidhaa hiyo muhimu. Aidha, viongozi hao wanasisitiza kuwa muungano kati ya UDA na ODM ungali imara.