Kenya inazidi kuendeleza mikakati ya uzalishaji wa kemikali aina ya ethanol kama njia inayoweza kuokoa sekta ya sukari inayoyumba, kwa kuiga mfano wa nchi ya Brazil. Kwenye mchakato huo, miwa hubadilishwa kuwa mafuta ambayo hupunguza gharama za mafuta, kuimarisha kawi na kubuni ajira.
Akizungumza wakati wa kongamano la 68 la Shirika la Kimataifa la Sukari huko Kwale, Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki na Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe walitangaza mabadiliko makubwa ya sera ambayo yanaweza kubadilisha miwa kutoka kuwa zao la chakula pekee hadi kuwa rasilimali muhimu ya nishati.