Takriban wakazi 500 wa Kapkonoin katika eneo bunge la Emgwen, kaunti ya Nandi, wamefanya maandamano wakilalamikia kuzuiwa kwa ujenzi wa barabara ya mtaa na baadhi ya mabwenyenye wenye ushawishi mkubwa katika kijiji Chao.
Wakazi hao walikusanyika asubuhi na mapema kabla ya kuandamana kuelekea eneo linalozozaniwa, wakisema wamechoshwa na changamoto wanazokumbana nazo kutokana na ukosefu wa barabara inayopitika hasa wakati wa dharura. Aidha wamesema kuwa wamejaribu kuchanga fedha kama jamii ili kufungua na kukarabati barabara hiyo ya mtaa, wakilenga kurahisisha usafiri wa wagonjwa, wanafunzi na shughuli za kila siku. Lakini juhudi zao zinakumbwa na pingamizi na vitisho kutoka mabwenyenye hao wanadaowa kuzuia ujenzi na kupanuliwa kwa barabara hiyo.