- 10,584 viewsDuration: 27:33BBC Africa Eye imepata nyaraka za polisi ambazo hazijawahi kuonekana hadharani pamoja na ushahidi wa kipekee, unaotoa mwanga mpya kuhusu mauaji ya mmoja wa wapelelezi mashuhuri zaidi nchini Afrika Kusini. Frans Mathipa aliuawa wakati akichunguza kutoweka kwa Abdalla Abadigga, anayedaiwa kuwa mwanamgambo wa Islamic State na pia chanzo cha taarifa za kijasusi. Wanachama saba wa kikosi maalum cha polisi (Special Forces) pamoja na mtu mwingine wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kuhusiana na mauaji ya Mathipa. Kati yao, saba wanakabiliwa pia na mashtaka, pamoja na watu wengine wanne, ya kumteka na kumuua Abadigga. Wote wanakanusha tuhuma hizo. Tazama uchunguzi wa BBC Africa Eye, “South Africa: Anatomy of a Cover Up,” kwenye kituo cha BBC News Africa YouTube na BBC iPlayer. #bbcswahili #BBCAfricaEye #uhalifu Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw