Kina mama washirikishwa katika vita dhidi ya ugaidi katika kaunti ya Garissa

  • | Citizen TV
    266 views

    Hatua ya kuwashirikisha kina mama katika vita dhidi ya ugaidi katika kaunti ya Garissa imetajwa kama njia bora zaidi ya kupambana na tatizo la kiusalama kwa kutumia vikundi vyao. Wakizungumza wakati wa kuzindua mpango utakaotumika na kina mama kutoka kaunti ndogo ya Dadaab kukabiliana na kero ya ugaidi, wakuu wa usalama na vikundi vya kijamii wamesema kina mama wana uwezo wa kutambua vikundi vinavyosajili vijana kwenye mitandao ya ugaidi kwa urahisi kutokana na kuwepo kwao vijijini kila mara. Aidha, serikali kwa upande wake imehaidi kuunga mkono juhudi hizo za kina mama hao kuhakikisha kuwa hali ya usalama imerejea katika maeneo ya mipakani.