Kinara wa Azimio asema maandamano kufanyika siku ya saba saba

  • | Citizen TV
    5,478 views

    Kinara wa Azimio Raila Odinga anasema kuwa Upinzani uko tayari kwa maandamano Ijumaa ya siku ya Saba Saba kulalamikia gharama ya juu ya maisha. Odinga ameikashifu serikali ya Kenya Kwanza, akidai kuwa Rais William Ruto ameliteka bunge nyara na kuhakikisha wabunge hawajali hali halisi ya mwananchi. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, viongozi wa upinzani wamekashifu semi kutoka kwa baadhi ya viongozi wakiitaka serikali kuheshimu masharti ya mahakama na kupunguza bei ya mafuta.