Skip to main content
Skip to main content

Kindiki ahakikisha uchaguzi wa 2027 utakuwa huru na wa haki

  • | Citizen TV
    1,874 views
    Duration: 1:36
    Naibu Rais Kithure Kindiki amewahakikishia Wakenya na washirika wa kimataifa kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 utakuwa huru, wa haki, wa amani na wa kuaminika. Akizungumza katika Mkutano wa 15 wa Ushirikiano wa Maendeleo katika makao yake rasmi Karen, Nairobi, Kindiki amesema serikali itafanya kila iwezalo kuhakikisha taifa linasalia imara wakati na baada ya uchaguzi. Aidha, Waziri Mkuu wa Baraza la Mawaziri Musalia Mudavadi amewaonya wanasiasa dhidi ya kusambaza taarifa zinazoweza kudhoofisha imani ya umma katika mchakato wa uchaguzi.