Skip to main content
Skip to main content

Kipkemboi na Kemuma watawala Nairobi Marathon

  • | Citizen TV
    187 views
    Enock Kipkemboi na Joy Kemuma ndio washindi wa makala ya mwaka huu ya mbio za Nairobi Marathon zilizofanyika jijini Nairobi. Kipkemboi alistahimili baridi kali ya asubuhi na kuibuka mshindi wa mbio hizo, akiwashinda Ronald Kwambai na Shadrack Kenduiywo waliomaliza katika nafasi ya pili na ya tatu mtawalia. Katika kitengo cha wanawake, Joy Kemuma aliibuka mshindi mbele ya Jacinta Chepkeoch na Nancy Jepleting, akitwaa ushindi wake wa kwanza mwaka huu baada ya kumaliza katika nafasi ya tano katika makala ya Eldoret. Mashindano hayo yalivutia zaidi ya wanariadha 17,500 kutoka mataifa 75, yakidhihirisha hadhi ya Nairobi Marathon kama mojawapo ya mbio kubwa zaidi katika eneo hili.