Wafanyabiashara na wakazi wa kongowea Mombasa watanufaika na huduma za kisheria na kuweza kuripoti visa vya dhulma za Kijinsia baada ya kuziduliwa kwa kituo kinacholenga kutoa msaada wa kisheria kwa wafanyabiashara na wakazi kupitia mahakama ya kushughulikia kesi ndogondogo.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo Mkurugenzi mkuu wa shirika la Sisters for justice Neila Abdallah,amesema Kituo hicho kinalenga kutoa ufahamu zaidi wa kesi ndogondogo na kuwawezesha waathiriwa kupata haki kwa urahisi . Hakimu wa mahakama ya kushughulikia kesi ndogondogo mjini Mombasa Wangeci Mwangi,amesema tangu kuanzishwa kwa mahakama hiyo mwaka 2022 wamerekodi zaidi ya kesi elfu 6 ambapo asilimia 97 ya kesi hizo zimesuluhishwa.