Kituo cha kuwatibu waraibu wa dawa za kulevya chafunguliwa eneo la Busia

  • | Citizen TV
    168 views

    Utumizi wa mihadarati miongoni mwa vijana umekuwa kero kubwa katika kaunti ya Busia huku dawa za kulevya zikihofiwa kuwa zinapenyezwa kupitia mianya kwenye mpaka wa Kenya na Uganda. Kuanzishwa kwa kituo cha kuwatibu waraibu w amihadarati katika eneo la Nambale kumefufua matumaini ya jamii inayoishi hapo kuwa vijana watakuwa na maisha mema baadaye.