Skip to main content
Skip to main content

Kizaazaa chashuhudiwa baada ya wakaazi kuvamia mkutano kuzuia ugavi wa ardhi tata Kajiado kusini

  • | Citizen TV
    401 views
    Duration: 1:21
    Kizaaza kilishuhudiwa baadaya maafisa wa kukabiliana na ghasiai, maafisa wa wizara ya ardhi Narok na maafisa katika ofisi ya naibu kamishna wa Narok kusini kulazimika kukimbilia usalama wao baada ya wakaazi wenye hamaki kutibua mkutano uliolenga kutekeleza amri ya korti ya kugaanya ardhi ya kijiji cha Enoosagami wadi ya Melelo, Narok kusini. Awali wahusika walikuwa wamefika chini ya ulinzi wa polisi kisha maombi maalum kufanywa ili kutatua mzozo huo unaohusisha takriban hekari 500. Licha ya kila upande kujieleza maafisa wa serikali walisisitiza kuwa sharti amri ya mahakama itekelezwe lakini wenyeji hao walipinga wakidai haki dhidi ya njama fiche ya mabwenyenye serikalini kunyakua ardhi hiyo. Takriban wakaazi 600 wanaishi eneo hilo ambalo utata wa umiliki wa ardhi umesalia changamoto kubwa kwa zaidi ya miaka 30.