Skip to main content
Skip to main content

Kizaazaa nje ya Bunge la Seneti huku Seneta Gloria Orwoba akizuiliwa kuingia

  • | Citizen TV
    12,694 views
    Duration: 2:45
    Kizaazaa kilishuhudiwa nje ya lango kuu la Bunge la Seneti baada ya seneta maalum aliyefurushwa na chama cha UDA, Gloria Orwoba, kuondolewa na maafisa wa polisi alipowasili kuhudhuria vikao vya Seneti. Orwoba alisisitiza kuwa yeye ni seneta, akitegemea uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa mwezi huu uliositisha kutimuliwa kwake hadi kesi ya kupinga uamuzi huo ikamilike. Gari la Orwoba alilolitumia kufunga lango la Bunge liliondolewa kwa nguvu, huku akizuiliwa na polisi baada ya kujaribu kujifungia langoni.