Shirika la Wafanyabiashara la Kenya KNCCI, limeitaka serikali kuweka mfumo jumuishi wa kodi unaowahusisha wafanyabiashara wote badala ya kuwalenga wachache, likionya kuwa hali hiyo inaleta ubaguzi na kuathiri biashara.
Wakikutana kwenye warsha hapa jijini nairobi, Wafanyabiashara na wawekezaji walisema utozaji wa ushuru kupita kiasi unaendelea kudumaza shughuli za kiuchumi. Mkurugenzi Mkuu wa KNCCI, Kenn Onditi, alisema KRA inapaswa kuwaelimisha Wakenya kuhusu ulipaji ushuru bila upendeleo, huku akisisitiza umuhimu wa uwazi katika sera za kodi ili kurahisisha mazingira ya biashara .