Skip to main content
Skip to main content

Kwa nini China inaongeza silaha za nyuklia?

  • | BBC Swahili
    43,497 views
    Duration: 2:47
    China inaongeza na kuboresha silaha zake za nyuklia kwa kasi kubwa sana. Ripoti za hivi karibuni za taasisi za kimataifa za utafiti wa amani na ulinzi zinaonyesha kuwa China ndiyo nchi inayopanua zana zake za nyuklia kwa kasi zaidi duniani kwa sasa. Makadirio yanaonyesha kuwa kati ya mwaka 2023 na 2025, China imekuwa ikiongeza takriban silaha 100 za nyuklia kwenye hifadhi yake kila mwaka. Hata hivyo, imekuwa ikificha na kutoweka wazi ukubwa wa hifadhi yake ya silaha za nyuklia na sera zinazohusiana nazo. #bbcswahili #china #nyuklia Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw