- 15,031 viewsDuration: 57sBenki kuu nchini Kenya imetoa ilani dhidi ya kutengenezwa kwa mashada ya maua kwa kutumia noti za nchi hiyo. Mtindo wa kutengeneza noti za pesa kama mapambo umeenea nchini Kenya hasa katika sherehe na hutumika kama zawadi. Kulingana na benki hiyo kuu, noti nyingi hukunjwa, husokotwa, kufungwa na pini na kushikanishwa na gundi jambo linazoziharibu. Lakini je ilani hiyo itakuwa na athari gani? Kwa mengi zaidi, jiunge naye @midababirye katika Dira ya Dunia TV leo saa tatu usiku kupitia ukurasa wetu wa YouTube wa BBC Swahili. #bbcswahili #kenya #maua Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw