Skip to main content
Skip to main content

KWS yakana kumteka nyara mvuvi Brian Odhiambo aliyepotea ndani ya Ziwa Nakuru

  • | Citizen TV
    252 views
    Duration: 2:01
    Shirika la huduma kwa wanyamapori nchini KWS limekanusha madai ya kumteka nyara mvuvi Brian Odhiambo. Mkurugenzi mkuu wa KWS Erastus Kanga akisema hakuna mgeni aliyeingia kwenye mbuga ya wanyamapori ya Ziwa Nakuru na kupotea kwa muda wa miaka kumi iliyopita. Baadhi ya walalamishi kutoka kaunti ya Nakuru wameitaka serikali kuhalalisha uvuvi katika ziwa hilo wakishikilia kwamba uvuvi umekuwa ukiendelea. Brian Odhiambo alionekana mwisho Januari mwaka uliopita, familia yake ikiiambia mahakama kwamba maafisa wa kws ndiyo waliokuwa naye mwisho. Walikuwa wakizungumza walipofika mbele ya kamati ya seneti ya usalama.