- 12,330 viewsDuration: 3:06Jioni ya leo tunaanzia hapa Nairobi, ambako mamia ya wakazi waliungana na viongozi wa Linda Mwananchi waliokuwa wakizunguka mitaa kadhaa ya jiji. Viongozi hao, wakiongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, wametangaza azma ya kufikia makubaliano ya kumpata mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya muungano huo dhidi ya Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu ujao. Na kama Seth Olale anavyoripoti, wanasiasa hao wameendelea kuikosoa serikali kwa kile wanachodai ni kushindwa kutekeleza ahadi zake kwa Wakenya.