- 2,786 viewsDuration: 1:40Ngamia kumi na wanne walikufa mapema leo kwenye ajali ya barabarani iliyotokea katika Barabara Kuu ya Namanga. Kulingana na mmiliki wa ngamia hao, ngamia wengine sita walipotea baada ya ajali hiyo na kwamba anakadiria hasara ya shilingi milioni nne. Polisi wanachunguza kilichosababisha ajali hiyo iliyohusisha lori la trela.