Serikali imeagiza maafisa wa mawasiliano ya umma kukabiliana na habari zisizo za ukweli, taarifa potovu pamoja na zile za uwongo kupitia uboreshaji wa jinsi idara mbalimbali na mashirika huwasilisha mipango pamoja na sera za serikali. Akihutubia kikao cha uhamasishaji cha mwasilianaji wa serikali jijini Nairobi hii leo, katibu wa utangazaji na mawasiliano Stephen Isaboke alitaka wawasilishaji wa mawasiliano ya umma kuelewa mabadiliko ya taarifa, kuthibitisha ukweli pamoja na kurahisisha habari za serikali kwa umma.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive