- 16,020 viewsDuration: 3:09Maafisa wanne wa polisi na wengine wawili wa KDF ni miongoni mwa washukiwa 10 waliofikishwa katika mahakama ya Milimani na Kajiado kwa madai ya kuhusika na wizi kwenye matukio mawili mjini Kitengela. Kwenye tukio la kwanza, maafisa wanne wa polisi wanadaiwa kumuibia raia wa Congo almasi na zaidi ya shilingi laki nne. Upande mwingine mjini humo, maafisa wawili wa KDF na washukiwa wengine wanne walikamatwa wakipanga kuvamia boma la afisa mmoja mkuu wa KDF, Jumatano alasiri.