- 1,589 viewsDuration: 3:15Haya yakijiri, Maafisa wanne wakuu wa serikali wanaohusishwa na sakata ya uagizaji mafuta, walifika tena katika idara ya Upelelezi wa Jinai kuhojiwa kuhusiana na uingizaji wa mafuta tata nchini. Maafisa hao wakifika mbele ya makachero mchana kutwa kueleza jinsi walivyoagizwa kutafuta mafuta zaidi nje ya mkataba wa serikali kwa serikali. Wakati huo huo, uchunguzi wa sakata hii ya mafuta umeendelea, huku watu 20 wakiwa tayari wameandikisha taarifa, akiwemo mkurugenzi wa kampuni moja ya mafuta nchini.