Maafisa wawili wanazuiliwa, kuwasilishwa mahakamani

  • | Citizen TV
    2,875 views

    Idara ya polisi jana iliagiza kukamatwa kwa afisa wa polisi aliyempiga risasi mchuuzi wa maski katikati mwa jiji la Nairobi. Taarifa kutoka idara ya polisi ikisema kuwa, imeghadhabishwa na tukio hilo la kupigwa risasi kwa raia ambaye hakuwa amejihami. Aidha taarifa hiyo ya punde zaidi imeitenga idara ya polisi dhidi ya makundi ya watu waliojihami walioonekana wakati wa maandamano jijini Nairobi.