- 287 viewsDuration: 1:19Mamia ya wakaazi wa eneobunge la Borabu kaunti ya Nyamira walifanya matembezi ya kutoa hamasisho kulalamikia pombe na dawa za kulevya katika eneo hilo. Wakibeba mabango, wenyeji wakiongozwa na makanisa ya Katoliki, SDA, pamoja na wawakilishi wa mashirika mbalimbali waliandaa msafara wa amani kutoka maeneo ya Nyaronde hadi Kijauri ambapo kikao cha umma kilifanyika. Maeneo haya yakitajwa kati yale yanayoongoza kwa pombe isiyoruhusiwa na mihadarati