Maandamano makubwa kuandaliwa tarehe 20 mwezi huu Nairobi

  • | K24 Video
    2,551 views

    Kinara wa Azimio Raila Odinga ametangaza kuanza rasmi kwa maandamano ya upinzani dhidi ya serikali ya rais William Ruto baada ya makataa yake ya siku 14 kukamilika bila ya rais kushughulikia matakwa ya Azimio. Raila aidha ametangaza tarehe 20 mwezi huu kuwa siku ya maandamano makubwa jijini Nairobi. Raila aliyeanzisha rasmi vuguvugu la kupigania demokrasia pia amesema kuwa na migomo na ususiaji wa kampuni zinazohusiana na serikali ya kenya kwanza.