Maaskofu wa kanisa katoliki wataka kulipwa deni la NHIF

  • | Citizen TV
    1,619 views

    Maaskofu wa kikatoliki sasa wanaitaka serikali kulipa shilingi bilioni mbili kama malipo ya hazina ya NHIF inayodaiwa na hospitali zinazoendeshwa na kanisa katoliki nchini. Maaskofu hawa wakisema wanataka pesa hizi kulipwa kabla ya mpito wa hazina mpya ya SHIF. Kwenye kikao na wanahabari, maaskofu hawa sasa wanasema huenda wanashindwa kutoa huduma za nafuu zinazotegemewa na wakenya wengi kwa uhaba wa vifaa na fedha