Ni afueni kw amagavana baada ya mahakama kuu kuamrisha wasijiwasilishwe kwa lazima katika bunge la seneti au kukamatwa na kuzuiliwa kwa kususia vikao vya seneti.
Agizo hilo limetolewa kwa seneti, polisi na bunge la kitaifa kufuatia mzozo kati ya maseneta na magavana kuhusu madai ya hogo wanapojiwasilisha kuhojiwa na kamati za seneti. agizo hilo litatekelezwa hadi pale kesi iliyowasilishwa itakaposikizwa na kuamuliwa. juma lililopita, kizaazaa kilishuhudiwa kwenye majengo ya bunge pale maseneta walipokuwa wakijaribu kumwasilisha gavana wa samburu kw apolisi. aidha polisi walikita kambi katika afisi za kaunti ya nairobi kw alengo la kumkamata gavana sakaja johnson kwa kukaidi vikao vya seneti.