Mahakama imemwachilia huru mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Ardhi, Mohammed Abdalla Swazuri, pamoja na wenzake kadhaa, katika kesi ya madai ya rushwa na malipo ya fidia ya ardhi ya shillingi million 221 ya shirika la reli la Kenya
Mahakama ilibaini kuwa upande wa mashtaka haukuthibitisha kesi yake kwa kiwango cha kisheria. Hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuonyesha udanganyifu au makusudi ya jinai kati ya washitakiwa. Aidha hakimu Eunice aliieleza kuwa ushahidi ulioonyesha kuwepo tofauti na mgongano wa kiutawala badala ya ukiukaji wa sheria.