- 3,954 viewsDuration: 29sPicha zilizorekodiwa kwa kutumia ndege isiyo na rubani (Drone) zimeonyesha 'michoro' ya ajabu inayotokana na maji taka yanayotiririka na kuingia katika ziwa Maharloo, lililopo kusini mwa Iran. Kwa mujibu wa mpiga picha, maji hayo ni mchanganyiko wa maji taka kutoka mijini na viwandani. Kwa miaka mingi, wanaharakati wa mazingira wamekuwa wakionya kuhusu uchafuzi wa ziwa hilo, ambalo ni makazi ya ndege wengi wanaohama kutoka maeneo mbalimbali duniani, wakiwemo flamingo na korongo. Mamlaka zimechukua hatua kadhaa kudhibiti uchafuzi huo, ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha kusafisha maji taka. #bbcswahili #iran #majitaka Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw