- 879 viewsDuration: 4:25Waathiriwa wa dhuluma za kijinsia na kimapenzi huko Tana River wanaendelea kuhangaika kila uchao. Na sio tu kutokana na dhuluma wanayopitia bali kwa kukosa usaidizi wa kutosha. Kaunti hiyo ni miongoni mwa zile zenye visa vingi zaidi vya dhuluma vinavyoripotiwa huku kiangazi na mafuriko yakichangia hali hii. Serikali na mashirika yasiyokuwa ya serikali yametakiwa kuongeza juhudi za kukabiliana na taswira hii.