- 155,897 viewsDuration: 1:52Makamu wa Rais wa Tanzania, Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa pamoja na utumishi wa umma. Katika barua aliyomwandikia Rais Samia Suluhu Hassan, Nchimbi amesema uamuzi huo umefanywa kwa mujibu wa Katiba na utaanza kutekelezwa Septemba 4, 2026. Taarifa za kujiuzulu kwake zimekuwa zikisambaa kwa wiki kadhaa, huku kukiwa na joto la kisiasa ndani ya CCM. Mpaka sasa hakuna mamlaka ya serikali iliyothibitisha rasmi taarifa hiyo, ingawa BBC imezungumza na vyanzo vyake vya ndani serikalini vilivyothibitisha taarifa hiyo, na vyombo vya habari vya ndani pia vimeripoti kuhusu uamuzi huo. Mwandishi wa BBC @frankmavura na maelezo zaidi #bbcswahili #tanzania #CCM #siasa #NchimbiEmmanue Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw