Skip to main content
Skip to main content

Makundi 35 ya wanawake yawezeshwa kiuchumi huko Mwangulu, Kwale

  • | Citizen TV
    152 views
    Duration: 1:57
    Gavana wa Kwale, Fatuma Achani, ameongoza hafla ya kuyawezesha makundi 35 ya kijamii huko Mwangulu, Wadi ya Mwereni, ili kukuza usawa wa kiuchumi na kupiga vita umaskini. Gavana amehimiza kina mama, vijana, na watu wenye ulemavu kujiunga na kuunda kampuni rasmi zitakazowawezesha kufuzu kupata zabuni za serikali. Tayari kampuni 490 zimeundwa, huku zaidi ya 200 zikifanikiwa kupata kandarasi, jambo linalolenga kuinua hali ya maisha ya wakazi wa Lungalunga na Kwale kwa jumla.