- 474 viewsDuration: 3:10Maelfu ya watu nchini wanapambana na malezi ya watoto wanaougua tawahudi. Ugonjwa huo unaathiri mawasiliano na jinsi wanaougua tawahudi wanatangamana na ulimwengu. Wanaoishi na tawahudi wanahitaji malezi maalum na matibabu ya akili, mwili na utangamano na jamii. Walezi hujipata katika hali ngumu ya kuwalea watoto hao kutokana na mahitaji yao maalum na unyanyapaa wa jamii.