- 1,259 viewsDuration: 3:36Waziri wa Afya Aden Duale ametangaza kusitishwa kwa malipo ya SHA kwa vituo 12 vya matibabu kutokana na ulaghai wa malipo ya huduma za SHA. Akizungumza mjini Garissa, Duale pia alitaja kaunti tano zinazoongoza kwa madai ya uwongo ya matibabu ya SHA, yakilenga kupata fedha kinyume cha sheria. Na kama anavyoarifu Mary Muoki, vituo 18 tayari vinakabiliwa na kesi mahakamani, huku idadi ya vituo vilivyositishwa tangu operesheni hiyo ianze ikifikia 1,000.