- 12,511 viewsDuration: 3:25Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya imekanusha madai kwamba kuna marufuku ya matumizi ya simu za bei nafuu nchini ambazo zinatumia chaja isiyokuwa ya 'type c'. Mamlaka hiyo ilitoa agizo kuwa kuanzia tarehe ishirini na nne mwezi huu wa machi, vifaa vyote vya simu za mkononi vinavyoletwa nchini viwe vyenye kutumia kichajio cha USB Type-C. Mamlaka hiyo imesema kuwa maelezo yake ni ya Kiufundi na haihusu vifaa ambavyo tayari viko nchini. Baadhi ya wakenya wana wasiwasi wa kukosa mawasiliano wakisema hawawezi kumudu gharama ya simu za aina hivyo huku wafanyibiashara wakihofia hasara.