Skip to main content
Skip to main content

Mapigano Transmara: Nyumba 200 zimeteketezwa, mamia watoroka Kilgoris

  • | Citizen TV
    1,937 views
    Duration: 1:22
    Hali ya taharuki imeendelea kutanda katika eneo la Angata Barrikoi kufuatia mapigano kati ya jamii zinazoishi eneo hilo. Taharuki hii ikizidishwa na visa vya kuteketezwa kwa baadhi ya nyumba katika wodi tatu za eneo hili la kaunti ya Narok.Picha kutoka vijiji hivyo zikionyesha baadhi ya nyumba zikiteketezwa, huku ripoti za serikali zikiarifu kuwa zaidi ya nyumba 200 katika wadi za Lolgorian, Keyian, Nkaararo na Angata Barikoi. zimechomwa. Awali kwenye kikao maalum na viongozi wa Narok, Gavana Patrick Ole Ntutu amesema kuwa mapigano hayo yamezidi kusambaa akilaumu baadhi ya viongozi kwa kuchochea ghasia hizi.