- 1,653 viewsDuration: 3:13Muungano wa raia kuhusu mageuzi ya sheria za uchaguzi unaoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu David Maraga, unataka kufutiliwa mbali kwa kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura za urais katika uchaguzi mkuu ujao. Muungano huo unasema kuwepo kwa kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura Bomas ni kinyume cha Katiba, ukilitaka IEBC kuheshimu matokeo ya mwisho ya kura yanayotangazwa katika vituo vya kupigia kura. Viongozi hao pia wanaitaka IEBC kufanya maboresho ya teknolojia ya uchaguzi na kuhakiki sajili ya wapiga kura kabla ya uchaguzi wa 2027.