Skip to main content
Skip to main content

Maraga: Gharama ya maisha itapanda mno kwa wakenya

  • | Citizen TV
    409 views
    Duration: 1:38
    Aliyekuwa Jaji Mkuu, David Maraga, ameikosoa serikali kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti za kuwalinda Wakenya dhidi ya ongezeko la gharama ya mafuta, akisema hali hiyo inaendelea kuathiri maisha ya wananchi wa kawaida. Akizungumza wakati wa ziara yake katika Kaunti ya Nandi, Maraga amesema kupanda kwa bei ya mafuta kumesababisha gharama ya maisha kupanda kwa kiwango kikubwa, hali inayowafanya Wakenya wengi kuishi kwa shida. Ameongeza kuwa licha ya changamoto hizo, serikali inaendelea kutenga fedha nyingi kwa Ofisi ya Rais badala ya kuangazia mahitaji ya msingi ya wananchi.