Marekani kuipa Kenya mamilioni ya dola

  • | K24 Video
    97 views

    Rais William Ruto ametaka ushirikiano zaidi kati ya Kenya na Marekani katika shughuli za kudumisha amani. Akizungumza baada ya kukutana na mwenyeji wake rais Joe Biden kwa mara ya kwanza katika ziara yake rasmi, Ruto ameishukuru marekani kwa kuwekeza kiwango kikubwa cha pesa katika miradi mbalimbali humu nchini. Rais Ruto anazuru Washington DC huku taifa la Kenya likijiandaa kuwapeleka maafisa wa polisi nchini haiti kudhibiti hali ya usalama.