Martha Karua aendeleza kampeni zake kaunti ya Tharaka Nithi

  • | K24 Video
    250 views

    Mgombea mwenza wa kinara wa Azimio, Martha Karua amewaonya vijana dhidi ya kutumika kuzua vurumai katika mikutano ya kampeni. Karua ambaye leo amekuwa akifanya kampeni katika maeneo ya kaunti ya Tharaka Nithi amewataka wapinzani wake kupambana naye ana kwa ana bila kutumia ovyo vijana ambao sio wana wao. Hii ni siku ya tatu ya muungano wa azimio ya kujinadi mlima kenya chini ya uongozi wa Karua.