- 21,379 viewsDuration: 1:56Je, viboko ni nyenzo muhimu ya kudumisha nidhamu au ni adhabu iliyopitwa na wakati? Mjadala huo umeibuka upya nchini Tanzania baada ya Mahakama Kuu kutoa uamuzi unaopiga marufuku adhabu ya viboko shuleni. Uamuzi huo umeibua maoni yanayokinzana kuhusu nafasi ya walimu katika kusimamia nidhamu na mbinu mbadala zinazoweza kutumika katika kumfundisha wanafunzi. Wewe una maoni gani? Je, unadhani wanafunzi wanaweza kufundishwa bila viboko? Mwandishi wa BBC @mariammjahid na taarifa hiyo Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw