Skip to main content
Skip to main content

Mashirika ya kijamii yapinga Mswada wa Fedha 2026, yaonya kuchukua hatua

  • | Citizen TV
    151 views
    Mashirika ya kijamii yameeleza upinzani wao kuhusu Mswada wa Fedha wa mwaka 2026, yakisema kuwa makato yaliyopendekezwa ni makubwa na Wakenya hawawezi kuyastahimili. Kupitia muungano wa Okoa Uchumi, mashirika hayo yamesema yana hofu kuwa mswada huo utaongeza mzigo wa madeni na ushuru kutokana na ongezeko la mikopo ya serikali. Sasa yameonya kuchukua hatua iwapo serikali haitasikiliza hoja zao.