- 682 viewsDuration: 1:13Siku chache baada ya Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen kuahidi kuimarisha usalama katika mpaka wa Kitui na Tana River, Seneta wa kuteuliwa Beth Syengo ameitaka serikali kuchukua hatua za haraka. Akizungumza katika eneo la Ngomeni, Mwingi Kaskazini, baada ya kugawa msaada wa chakula, Syengo alitoa wito kwa serikali kuboresha hali ya maisha ya askari wa akiba kwa kuwaongezea marupurupu. Kulingana naye, polisi hao hupokea marupurupu kidogo mno ikilinganishwa na kazi yao.