- 65,979 viewsDuration: 2:37Mwaka mmoja baada ya maandamano na ghasia kubwa zilizofuatia uchaguzi wa Oktoba 2025 nchini Tanzania, familia zinaendelea kuomboleza wapendwa wao waliouawa katika machafuko hayo, huku manusura wengine wakiishi na majeraha yaliyobadilisha maisha yao ikiwa ni pamoja na kushindwa kujigharamia matibabu. Ripoti mpya ya Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International imeishutumu serikali kwa kushindwa kuwawajibisha waliohusika na vifo vya waandamanaji jambo ambalo serikali ya Tanzania imekua ikikanusha. Mamlaka nchini Tanzania hazikujibu ombi la BBC la kuhusu madai hayo. Mwandishi wetu Alfred Lasteck amezungumza na familia ambazo bado zinatafuta haki na majibu kuhusu wapendwa wao waliopotea #bbcswahili #tanzania #oktoba29 Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw