- 177 viewsDuration: 1:39Mbunge wa Ndaragwa George Gachagua amezitaka shule za umma katika eneo hilo kukumbatia kikamilifu mafunzo ya kidijitali. Mbunge huyo amesisitiza umuhimu wa kutumia rasilimali za kiteknolojia shuleni, kwa kuwapa wanafunzi ujuzi unaohitajika ili kukabiliana na changamoto za elimu ya kisasa na kuwatayarisha kwa siku zijazo. Amezungumza wakati wa hafla ya kufungua jengo la ofisi ambalo pia litatumika kama maktaba ya kidijitali katika shule ya Upili ya Karagoine, Ndaragwa.