- 3,781 viewsDuration: 1:20Rais William Ruto na Spika wa bunge la taifa Moses Wetangula wameongoza Wakenya kumuomboleza mbunge wa Ol Kalou. David Njuguna Kiaraho aliyeaga dunia usiku wa kuamkia leo. Familia iliyotangaza kifo chake imesema kuwa mwanasiasa huyo almekuwa akiugua kwa muda na alikuwa akipokea matibabu katika Nairobi Hospital. Rais na Spika wa bunge la kitaifa wamemtaja Kiaraho kama kiongozi shupavu aliyejali maslahi ya wanyonge. Aidha, wakazi wa Ol Kalou waliojawa na huzuni walijitokeza kuifariji familia nyumbani kwake katika kaunti ya Nyandarua.