Mchuuzi aliyepigwa risasi afanyiwa upasuaji

  • | Citizen TV
    5,232 views

    Mchuuzi aliyepigwa risasi na polisi katikati mwa jiji la nairobi bado yu hai na anapokea matibabu katika hospitali ya kitaifa ya kenyatta. Familia yake baada ya kumtembelea katika chumba cha ICU katika hospitali ya Kenyatta imeelezea kuwa Boniface Mwangi Kariuki anaendelea kupigania maisha yake. Usimamizi wa hospitali ya kenyatta nao ukisema madaktari wanafanya kila wawezalo, baada ya kumfanyia upasuaji kwa saa mbili.