- 196 viewsDuration: 1:04Wanafunzi wanaoishi na ulemavu wa kuona katika kaunti ya kitui wamepokea mafunzo ya michezo mbalimbali kutoka kwa shirika la tucheze kama njia ya kukuza talanta za watu wenye mahitaji maalum. Mpango huo ambao pia unalenga walimu zaidi ya 80 kutoka maeneo yote nchini kwenye michezo ya goal ball na sound ball. Shule zote ambazo ziko chini ya mpango huo wa tucheze hupokea vifaa vya michezo ikiwemo mipira maalum , huku lengo kuu likiwa kuwafikia jumla ya wanafunzi 4,000 kote nchini.