Skip to main content
Skip to main content

Miradi ya maji ya gharama ya Ksh.1.7b yaelekea kukamilika Machakos

  • | Citizen TV
    180 views
    Duration: 1:49
    Wakaazi zaidi ya laki moja unusu katika kaunti ya Machakos wanatarajiwa kupata maji kwa wingi ya miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.7 inayokaribia kukamilika. Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi hiyo, Waziri wa Maji Eric Muriithi Mugaa alisema utekelezaji wa miradi hiyo umefikia asilimia 93 na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi miwili ijayo. Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa Mwala, utakaotoa maji kutoka mto Ndarugu kaunti ya Kiambu na kusambaza lita milioni 6.6 kila siku .