- 7,922 viewsDuration: 3:33Serikali imeanzisha miradi ya zaidi ya shilingi bilioni 10 katika eneo bunge la Ol Kalou huku uchaguzi mdogo wa eneo hilo ukitarajiwa wiki ijayo. Leo, Katibu wa Idara ya Uchumi wa Baharini na Maziwa, Betsy Muthoni, aliongoza hafla ya kuzindua boti mbili zenye thamani ya shilingi milioni tano kwa wakazi wa Ol Kalou. Hafla hiyo imefanyika siku moja baada ya Katibu wa Idara ya Nishati Alex Wachira na aliyekuwa Waziri Moses Kuria kugawa mitungi 20,000 ya gesi ya kupikia kwa wakazi wa eneo hilo. Hata hivyo, upinzani umedai kuwa hatua hizo ni mbinu ya serikali ya kuwahonga wapiga kura kabla ya uchaguzi mdogo.